Vigezo na Masharti ya Karo (Terms & Conditions)

Last Updated: January 20, 2026

Utangulizi:

Karibu Karo. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubaliana na masharti haya. Karo ni soko la kidijitali linalounganisha Wauzaji na Wanunuzi nchini Tanzania.

A. Majukumu ya Karo:

Karo ni jukwaa (platform) tu. Hatumiliki bidhaa zinazouzwa na wauzaji binafsi.

Tunajitahidi kuhakikisha usalama wa miamala, lakini hatuwajibiki moja kwa moja kwa ubora wa bidhaa kutoka kwa muuzaji.

B. Majukumu ya Muuzaji (Vendor):

Muuzaji lazima aweke picha na maelezo halisi ya bidhaa.

Ni marufuku kuuza bidhaa haramu, zilizoibwa, au feki.

Muuzaji anapaswa kukamilisha oda ndani ya muda uliopangwa.

C. Malipo na Bei:

Bei zote ziko katika Shilingi ya Tanzania (TZS).

Malipo yanaweza kufanyika mtandaoni au wakati wa kupokea bidhaa (Cash on Delivery) kulingana na makubaliano ya bidhaa husika.

D. Sera ya Kurudisha Bidhaa (Returns & Refunds):

Mteja ana haki ya kurudisha bidhaa ndani ya siku 3 ikiwa ina hitilafu au siyo ile aliyoagiza.

Bidhaa lazima iwe katika hali ile ile iliyopokelewa (isitumike au kufunguliwa nembo).

E. Sheria Inayotumika: Masharti haya yanasimamiwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.